TUTARAJIE NINI KWENYE '911' ALBAMU MPYA YA NANDY? — THE AFRICAN PRINCESS ANAPOKUWA ZAIDI YA BONGO FLAVA

Miaka minane imepita tangu Nandy alipotoa The African Princess, album iliyomweka rasmi kwenye ramani ya Bongo Fleva ikiwa na nyimbo kama Aibu, Hazipo, One Day, Kivuruge na Ninogeshe. Tangu hapo, Nandy hakukaa kimya; ametoa EP kadhaa, singles, kolabo za ndani na nje ya Tanzania, ameanzisha label yake na kujenga Nandy Festival kama mali yake mwenyewe. 


Na Januari 2026, Nandy aliwaambia mashabiki kwamba angeachia album mbili ndani ya mwaka 2026—moja baada ya Ramadhan na nyingine kuelekea mwisho wa mwaka. 

Kwa hiyo swali sasa sio tu “Nandy atatoa album gani?”

Swali kubwa zaidi ni:

“The African Princess anataka kuwa nani baada ya album hii?”

1. Tunatarajia Nandy mwenye African Identity zaidi.

Kuna sababu ya kuangalia muelekeo huu.

Nandy tayari amekuwa na historia ya kuvuka mipaka ya Tanzania. Alishiriki Coke Studio Africa 2017 akiwa ameunganishwa na Betty G wa Ethiopia, na baadaye amekuwa na kolabo na wasanii kutoka Nigeria, Kenya na South Africa. Napona alimshirikisha Oxlade wa Nigeria, wakati Let It Go ilimunganisha na Kingdmusic wa South Africa kwenye project ya Pan-African ya ZiiBeats. 

Na mwaka 2026 pattern hiyo haijaonekana kupungua.

Tumemuona kwenye Somebody na Marioo, Malaika na Mbosso chini ya production ya S2Kizzy, pamoja na releases nyingine zinazopanua lugha na muonekano wa muziki wake. Malaika yenyewe imeelezewa kama Afro-pop/Bongo Flava yenye mizizi ya Afrika Mashariki. 

Hivyo, tunaposema African connection, sio lazima iwe album iliyojaa kolabo za Nigeria pekee.

Inaweza kuwa Nandy akitengeneza muziki ambao unasikika Afrika Mashariki kwa utambulisho, lakini Kiafrika kwa mwenendo.


2. Kuna uwezekano wa sound yake kuondoka kwenye “Nandy formula” ya zamani

Nandy wa One Day na Nagusagusa alitambulika kwa nguvu ya melody, vocals na Bongo Flava yenye identity ya wazi. Lakini catalog ya miaka ya hivi karibuni inaonyesha alikuwa akigusa Afro-pop, sound za kisasa za Kiafrika na kolabo zenye watayarishaji na wasanii kutoka maeneo tofauti. 


Let It Go ilikuwa na Kingdmusic na ZiiBeats. Wahala ilimkutanisha na Khanyisa. Malaika inamkutanisha na Mbosso na S2Kizzy. Hizi si kolabo za ilimradi; kwa pamoja zinaonyesha Nandy amekuwa akijenga vocabulary pana zaidi ya sound. 


Kwa hiyo utabiri wetu wa kwanza ni huu;


Album ijayo inaweza isiwe “Nandy akiwa amerudi kufanya Bongo Flava.” Inaweza kuwa Nandy akitumia Bongo Flava kama msingi wa sound kubwa zaidi ya African pop.


3. Tunapaswa kutarajia collaborations zenye mikakati zaidi


Album ya kwanza ya Nandy ilikuwa tofauti sana na albumu nyingi za Bongo Fleva za sasa. The African Princess ilikuwa project iliyobeba utambulisho wake kwa nguvu, huku ikiwa na kolabo chache sana. 


Leo Nandy ana network pana zaidi.


Ana historia na Oxlade, Kingdmusic, Jux, Marioo, Mbosso, Alikiba, Harmonize na wengine, huku akiwa ameshafanya kazi katika mazingira ya Pan-African kupitia Coke Studio na ZiiBeats. 


Kwa hiyo kama album hii itakuwa na collaborations nyingi, kitu cha kuvutia haitakuwa idadi ya kolabo.


Itakuwa ni nani anachagua kumleta kwenye dunia yake — na kwa nini.


4. Album hii inaweza kuwa “brand statement” ya The African Princess


Hapa ndipo stori inakuwa kubwa kuliko muziki.


Nandy sasa sio msanii wa kurekodi tu.


Ana Nandy Festival, ana The African Princess label, na ameweka wazi kwamba anaangalia biashara ya muziki kupitia ushirika wa kimkakati.


Nandy mwenyewe alisema kwamba alipounda The African Princess label, vision yake haikuwa Tanzania tu, alieleza nia ya kuifanya iwe jukwa la wasanii wa kike kutoka sehemu mbalimbali za Africa. 


Kwa hiyo album mpya inaweza kufanya kitu kingine:


kuipa maana mpya title “African Princess.”


2018 ilikuwa ni utambulisho.


2026 inaweza kuwa mwaka wa ongezeko;

Kutoka kuwa jina la msanii → kuwa utambulisho wa muziki, utambulisho wa kibiashara na kuingia miongoni mwa wasanii wanaotangaza utamaduni wa Kiafrika


5. Nandy Festival inaweza kuwa sehemu ya kuelewa album hii


Nandy Festival ya 2026 imekuwa ikitumika pia kusherehekea miaka 10 ya safari yake kwenye muziki, na imejengwa kama touring festival inayokwenda miji mbalimbali. 


Hii inafanya album inayokuja kuwa interesting zaidi kwa sababu Nandy sasa ana kitu ambacho hakuwahi kuwa nacho wakati wa album ya kwanza:


Ana audience yake mwenyewe.

Ana streaming fanbase.

Ana social audience.

Ana live audience.

Ana festival.

Ana label.

Ana brand.


Kwa hiyo album hii inaweza kuwa zaidi ya mkusanyiko wa nyimbo.


Inaweza kuwa soundtrack ya era mpya ya The African Princess.


Na utabiri mkubwa zaidi?


Bongo Review inaona nafasi kubwa ya Nandy kutafuta uwanja wa kuchezea kati ya Bongo Flava yake na African pop ya nje.


Sio kuiga Afrobeats.


Sil kuachana na Kiswahili.


Sio kufuata Amapiano kwa sababu ni trend.


Bali kuchukua kile ambacho tayari ni chake—sauti, melody, nguvu ya mwanmke, hisia, na simulizi zame —na kuweka kwenye production na kolabo ambazo zinaweza kusafiri zaidi ya Tanzania.


Kwa sababu baada ya miaka 10 kwenye industry, hatuulizani tena kama “anaweza kuwa star?”. Hilo tayari amelijibu.


Swali la album hii litakuwa:


>“The African Princess anaweza kujenga sound yenye utambulisho ambao watu wa Africa nzima wataitambua kuwa ni yake?”


Na hapo ndipo album hii inaweza kuwa na maana kubwa zaidi kwenye career yake.


2018: The African Princess alijitambulisha.

2026: The African Princess anaweza kuwa anajipanua.


Tutegemee nini? More Africa. Bigger collaborations. Na zaidi ya yote — Nandy anayefanya identity yake ya “African Princess” kuwa movement, sio jina la stejini peke yake.

Post a Comment

0 Comments