DRAKE VS UMG: KESI YA “NOT LIKE US” YAENDA TENA MAHAKAMANI DESEMBA

Mzozo wa kesi kati ya Drake na Universal Music Group (UMG) kuhusu wimbo wa Kendrick Lamar, “Not Like Us,” haujaisha.

Mahakama ya Rufaa ya Marekani imepanga kusikiliza hoja za pande zote mbili Desemba 4, 2026, kwenye hatua inayofuata ya rufaa ya Drake dhidi ya uamuzi ulioutupilia mbali kesi yake mwaka jana.

Drake aliishtaki UMG Januari 2025, akidai kuwa kampuni hiyo ilihusika katika kusambaza na kuutangaza “Not Like Us” licha ya madai aliyosema yalikuwa ya uongo na yenye kumchafulia jina.


Kendrick Lamar sio mshtakiwa kwenye kesi hii. Drake ameilenga UMG kwa namna ilivyoshughulikia na kuutangaza wimbo huo.


Oktoba 2025, Jaji Jeannette Vargas wa Southern District of New York alifuta madai yote ya Drake. Mahakama ilisema kauli zinazolalamikiwa kwenye “Not Like Us” zilikuwa ni maoni ambayo hayawezi kuwa msingi wa madai ya kuchafuliwa, kwa kuzingatia mazingira ya rap battle ambayo wimbo ulitoka. Mahakama pia ilisema msikilizaji wa kawaida asingeelewa wimbo huo kama unaowasilisha ukweli kuhusu Drake. Kwenye rufaa yake, mawakili wa Drake wanapinga tafsiri kwamba diss tracks zinapaswa kuchukuliwa kama maoni tu.Wanasema uamuzi wa mahakama ya chini uliweka kile wanachokiita kauli zinazotolewa kwenye rap diss track haziwezi kuchukuliwa kama statements of fact zinazoweza kusababisha kesi ya defamation.


Kwa upande mwingine, UMG inataka uamuzi wa mwanzo ubaki palepale. Kwenye hoja zake, kampuni hiyo inasisitiza kwamba maneno ya “Not Like Us” hayawezi kutenganishwa na mazingira ya rap battle, ambayo yana sifa ya udhalilishaji.

Pia kuna swali pana kuhusu mipaka ya uhuru wa kisanii kwenye muziki:

Ikiwa msanii anatoa madai makali nd NIani ya diss track, ni wakati gani maneno hayo yanachukuliwa kama sehemu ya sanaa na battle rap — na ni wakati gani yanaweza kuchukuliwa kama madai ya ukweli yanayoweza kusababisha uwajibikaji wa kisheria?

Kwa sasa, “Not Like Us” bado inaendelea kuleta matokeo nje ya muziki wenyewe — kutoka kwenye beef ya Drake na Kendrick hadi kwenye mjadala kuhusu nguvu za labels, reputation ya wasanii na mipaka ya sanaa inapokutana na sheria.

Post a Comment

0 Comments