ABIGAIL CHAMS ATEULIWA KUWA BALOZI WA TAIFA WA UNICEF TANZANIA
Abigail Chams amethibitishwa rasmi kuwa Balozi wa Taifa wa @uniceftz hatua kubwa inayoongeza kwenye orodha yake ya mafanikio, sasa akichukua jukumu linalojikita kwenye kubadilisha maisha ya watoto na vijana nchini.
Kama Balozi wa Taifa, Abigail atatumia sauti yake kuangazia mada nzito kama afya ya akili, ukatili dhidi ya watoto, na masuala mengine ambayo vijana mara nyingi hukuta vigumu kuyazungumza. Lengo lake kuu ni kuwahamasisha watoto na vijana kusema wazi na kutafuta msaada wanapouhitaji.


0 Comments: