STEPPA SASA INAVALIKA: AIKA NA NAHREEL WANAANZA KUGEUZA ALBAMU KUWA BRAND

Aika na Nahreel wamefanya kitu ambacho kinaweza kuonekana kidogo kwa macho, lakini kina maana kubwa kwenye music business: wamechukua STEPPA kutoka kwenye streaming platforms na kuipeleka kwenye maisha ya mashabiki wao.

Wiki chache baada ya kuachia album hiyo, duo imeanza kuuza rasmi STEPPA merchandise kupitia platform yao wenyewe — T-shirts, tote bags, caps na notebooks.

Hii si tu suala la kuuza nguo.

Ni hatua ya kugeuza album kutoka kuwa content inayosikilizwa kuwa identity inayoweza kumilikiwa na shabiki.


Kutoka Album Hadi Brand

Kinachovutia zaidi ni namna merchandise hiyo inavyotumia identity ya STEPPA.

T-shirt hazina tu artwork ya album. Tracklist yote ya nyimbo 10 imewekwa nyuma kwa mfumo wa 1/10 hadi 10/10.

Kwa hiyo shabiki hanunui tu T-shirt yenye jina la wasanii, anavaa album yenyewe.

Hapo ndipo music na fashion zinapoanza kukutana. Audience Inaanza Kuwa Commercial Asset. Kwa msanii, streaming ni njia moja ya monetization. Live performance ni nyingine. Brand partnerships ni nyingine. Lakini merch inafungua channel nyingine: fan-to-artist commerce.


Shabiki anayependa STEPPA anaweza kuisupport bila ku-stream wimbo mwingine.

Anaweza kununua T-shirt. Anaweza kununua kofia. Anaweza kubeba bag. Anaweza kuhifadhi notebook.

Na kila bidhaa inakuwa pia mobile marketing ya album.

Mtu akivaa T-shirt ya STEPPA mjini, album inapata impression nyingine nje ya Spotify, Apple Music au YouTube.

Lakini Move Kubwa Iko Kwenye Direct-to-Fan

Merchandise kupitia website yao wenyewe pia inafungua conversation muhimu kuhusu artist ownership.

Kadiri msanii anavyoweza kujenga relationship ya moja kwa moja na fan, ndivyo anavyoweza kuelewa vizuri zaidi audience yake, bidhaa wanazotaka na namna wanavyotaka ku-support career yake.

Hapa ndipo STEPPA inaanza kuonekana kama music property, si collection ya nyimbo 10 tu. Na Hii Ndiyo Hatua Ambayo Bongo Flava Inapaswa Kuiangalia

Swali sasa sio;

“Album ime-stream mara ngapi?”

Ni pia:

“Album imeunda nini ambacho mtu yuko tayari kukimiliki?”

Kwa sababu biashara haishii kwenye kuuza muziki.

Unauza experience.

Unauza identity.

Unauza uwepo.

Aika na Nahreel wameanza kujaribu hilo kupitia STEPPA.

Bado hatuna data ya mauzo ya merch hii, hivyo haiwezekani kusema tayari imekuwa success ya kibiashara.


Lakini direction yenyewe inaonyesha kitu muhimu:

Album inaweza kuwa mwanzo wa biashara nyingine nyingi — ikiwa msanii anaijenga kama brand, si release tu.

STEPPA sasa haisikilizwi tu.

STEPPA inavaliwa

Post a Comment

0 Comments